Captain Smyzy - Majuto Lyrics

  • Artist/Band:
  • Album:
  • Song Title:
  • Text Options:
  • Share & Like:

....yeah, thiz about life man.
....(chiness bizness) Every thing you do,
Fikiria, hujui place utaishia...au sio
verse 1
Skiza story yake, mwana wa mabepari
toka alipozaliwa hali yake ilikuwa shwari
kama mtoto yeyote aliishi na wazazi
na alipotak chochote alitegemea wazazi
hizo hela za babake zilimpa ujeuri
hakuna mtu yeyote aloweza kumshauri
wote aliwachukua tu kama watu mabwege
bila kujua hatimaye hali yake itakuwaje
wazazi walimpenda mshkaji kaanza kudeka
kajiona ameshafaulu shuleni akatoweka
kajiunga na vikundi haram wakamchombeza
mi nashindwa kwani hakufaham watampoteza?
mshkaji alizidisha vituko kila kukicha
leo kaiba mbuzi kesh okuku kamficha
kapelekwa kwa chief, ili apate kumkashif,
hapo bado kaishia kumtongoza mke wa chifu.
Chorus
Nilimuonya lakini hakusikia

aliona kama mimi siwezi kumsaidia
cheki sasa hatimaye anajutia
vitu alivofanya ndo sa' vinamchukia x2
verse 2
Zilipita siku chache hali ikizidi kuwa mbaya
bwana chifu kampitisha kwenye koti za wilaya
mateso aloyapata siwez kusimulia
na mpaka siku ya leo bado nazifikiria
alifanywa atembee huku amefungwa miguu
wakamweka kwenye celi akisubiri siku kuu
back at home, watu walishachoka naye
mpaka wazazi wake walishachoka kuishi naye
siku ilipowadia alipelekwa mahakamani
kesi yake iliposikizwa alihukumiwa maishani
cheki sasa anajuta, nafsi inamsuta
kwani yeye ndo chanzo kwa yale yote yalomkuta
sina uwezo wowote mie wa kumsaidia
nilimuonya mara mia kaniona kama gunia
so, peace for life, namalizia story yangu
asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu.
chorus x2

Search Song Lyrics
Browse Artists

A B C D E F G H I J K L M N
O P Q R S T U V W X Y Z #

Hide preview
Lyrics and Video Widget:

Code for your site/blog/space

Click above to select the code then right click & copy to get the code to paste onto your site/blog